SEHEMU YA KUMI NA MBILI
SIMULIZI: HATIA TAKATIFU
Mwandishi: Kedmund Mtembezi
Email kedmund742@gmail.com
WhatsApp+255 672 229 424
SEHEMU YA 12
Usiku ule uliacha alama.
Baada ya tukio la ghala, kila upande ulijipanga upya.
π Rashid alikuwa na hasira.
π Mzee alikuwa anaangalia mchezo kwa mbali.
π Na Kedmund… alikuwa anajenga nguvu zake kimya kimya.
Asubuhi iliyofuata, Kedmund hakurudi nyumbani.
Alihamia kwenye sehemu ya siri — jengo lililokuwa limeachwa, lakini ndani yake kulikuwa na mipango mipya.
Watu wachache waliokuwa waaminifu walikuwa pembeni yake.
Sasa hakutaka kundi kubwa.
π Alitaka watu wachache… lakini hatari.
“Kuanzia leo, hatufanyi kazi kwa hofu,” Kedmund alisema.
Wote walimwangalia.
“Tunafanya kazi kwa akili.”
Alitoa ramani mezani.
“Rashid ana vituo vitatu vya biashara.”
Alionyesha kwa kidole:
Ghala la mzigo
Sehemu ya pesa
Njia ya mawasiliano
“Tukivunja hivi… atapoteza nguvu.”
Mmoja wa watu wake aliuliza:
“Tutaanza wapi?”
Kedmund alitabasamu kidogo.
“Pale ambapo ataumia zaidi.”
π Pesa.
Wakati huo huo…
Rashid alikuwa amekaa ndani ya ofisi yake, akivuta sigara kwa hasira.
“Huyo kijana anafikiri amekua sana,” alisema.
Mmoja wa watu wake akasema:
“Tumtafute na tumalize.”
Lakini Rashid alitikisa kichwa.
“Hapana… nataka aumie kwanza.”
Macho yake yakawa makali.
“Tutamchukua mtu wake wa karibu.”
Jina moja lilipita akilini mwake.
π Amina.
Usiku ulipoingia…
Kedmund na kundi lake walikuwa tayari.
Walivaa nguo nyeusi, wakajipanga kimya kimya.
Hakukuwa na kelele.
Hakukuwa na makosa.
π Hii ilikuwa mission ya kwanza ya vita.
Walifika kwenye jengo la kuhifadhi pesa.
Ulinzi ulikuwa mkali… lakini si kwa Kedmund.
“Camera iko wapi?” aliuliza.
“Upande wa kulia,” mmoja alijibu.
Kedmund alitikisa kichwa.
“Dakika mbili… tuingie.”
Kwa ustadi mkubwa, waliingia ndani.
Hakuna kelele.
Hakuna alarm.
π Precision.
Ndani…
walikuta pesa.
Nyingi.
Mifuko.
Maboksi.
Ndoto za watu wengi.
Lakini Kedmund hakutabasamu.
Hii haikuwa kuhusu utajiri.
π Ilikuwa ni ujumbe.
“Chukua sehemu… lakini choma iliyobaki,” alisema.
Watu wake walishangaa.
“Boss… pesa yote hii?”
Kedmund aliwatazama.
“Sitaki tu pesa… nataka kumuumiza.”
Dakika chache baadaye—
π₯ MOTO ULILIPUKA!
Jengo likaanza kuwaka.
Mosho ulipanda juu.
Ilikuwa ishara.
π Vita imeanza rasmi.
Wakiwa wanatoroka, Kedmund alisimama kwa sekunde moja, akitazama moto.
Macho yake yalikuwa na baridi.
“Game on…” alisema taratibu.
Lakini hakujua…
Wakati huo huo…
Amina alikuwa kwenye gari.
Amefungwa mikono.
Akiwa amechukuliwa na watu wa Rashid.
Macho yake yalikuwa na hofu… lakini pia uamuzi.
Simu ya Kedmund iliita.
Alipoipokea—
sauti ya Rashid ilisika.
“Umeanza moto… sasa angalia ninachofanya.”
Kimya kilitanda.
“Kama unamtaka Amina hai…”
Moyo wa Kedmund ulisimama kwa sekunde.
“Njoo peke yako.”
Call ikakatika.
Ndani ya sekunde chache, kila kitu kilibadilika.
π Vita haikuwa tena kuhusu biashara.
π Sasa ilikuwa binafsi.
Watu wake walimwangalia.
“Boss… plan?”
Kedmund alikaa kimya kwa sekunde chache.
Kisha akasema:
“Hi ni trap.”
“Basi tusifanye—” mmoja alisema.
Kedmund alikata.
“Tutafanya.”
Macho yake yalibadilika tena.
π Hasira
π Uamuzi
π Na kitu kingine hatari zaidi…
π Upendo uliogeuka kuwa vita.
“Lakini safari hii…” alisema polepole,
π “Tutakuwa tayari kwa kila kitu.”
Mwisho wa Sehemu ya 12
Tukutane sehemu ya 13.
Maoni
Chapisha Maoni