SEHEMU YA TANO

 SIMULIZI: HATIA TAKATIFU


Mwandishi: Kedmund Mtembezi


Email kedmund742@gmail.com

WhatsApp+255 672 229 424


SEHEMU YA 5


Usiku ulikuwa tulivu, lakini ndani ya moyo wa Kedmund kulikuwa na kelele nyingi.

Alikuwa amekaa nje ya nyumba yao, akitazama anga lililojaa nyota. Lakini hakuziona vizuri… kwa sababu akili yake ilikuwa kwa mtu mmoja tu.

Amina.

Tangu walipoanza kuongea, maisha yake yalibadilika kwa namna nyingine kabisa. Sio pesa, sio kazi… bali hisia.

Kwa mara ya kwanza tangu aingie kwenye huu mchezo, alihisi kama kuna kitu kinampa sababu ya kuendelea.

Lakini hakujua…

Sababu hiyo hiyo inaweza kuwa mwisho wake.

Simu yake iliita.

Ilikuwa ni Amina.

“Uko wapi?” aliuliza kwa sauti laini.

“Nyumbani… natulia tu,” Kedmund alijibu.

“Nahitaji kukuona.”

Moyo wake uliruka.

“Sasa hivi?”

“Ndiyo… ni muhimu.”

Hakukuwa na maswali mengi.

Ndani ya dakika chache, Kedmund alikuwa njiani.

Walikutana sehemu tulivu, mbali na kelele za mtaa. Taa za barabarani zilikuwa zinawamulika kwa mwanga hafifu.

Amina alionekana tofauti kidogo leo.

Hakuwa na ile confidence yake ya kawaida.

“Kuna shida?” Kedmund aliuliza.

Amina alikaa kimya kwa sekunde kadhaa… kisha akasema:

“Kedmund… hii maisha si salama kama unavyofikiria.”

Kedmund alimtazama.

“Najua… lakini nipo tayari.”

Amina alitikisa kichwa kidogo.

“Hapana… hujui unachoingia.”

Kulikuwa na ukimya mfupi.

“Kuna watu wanakuangalia,” Amina aliendelea. “Na sio wote wanataka ufanikiwe.”

Moyo wa Kedmund ulianza kupiga kwa kasi.

“Una maana gani?”

Amina alimtazama machoni… lakini safari hii macho yake yalikuwa na huzuni.

“Ukikaribia sana juu… watu wanataka kukuangusha.”

Wakati huo huo…

Mbali kidogo, gari moja lilikuwa limeegeshwa gizani.

Ndani yake kulikuwa na wanaume wawili.

“Mzee alisema tuwafuatilie,” mmoja alisema.

Yule mwingine alitabasamu vibaya.

“Leo tutapata majibu.”

Kedmund hakuwa na idea.

Alikuwa bado amekaa na Amina.

“Unaniogopa?” aliuliza kwa utani kidogo.

Amina hakutabasamu.

“Naogopa kukupoteza,” alisema polepole.

Maneno hayo yalimpiga Kedmund moja kwa moja moyoni.

Alimsogelea karibu.

“Hautanipoteza.”

Kwa sekunde chache…

walikuwa karibu sana.

Lakini ghafla—

🔊 MLIO WA GARI!

Mwanga mkali ukawamulika.

“Mshuke hapo hapo!” sauti kali ilisikika.

Kedmund aligeuka kwa haraka.

Wanaume wawili walikuwa wanakuja kwa kasi kuelekea kwao.

“Run!” Amina alipaza sauti.

Hakukuwa na muda wa kufikiria.

Walikimbia.

Moyo wa Kedmund ulikuwa unapiga kwa nguvu kuliko wakati wowote ule.

Walikuwa wanapita kwenye njia za giza, wakikimbia bila kuangalia nyuma.

“Ni nani hao?!” Kedmund aliuliza huku akikimbia.

Amina hakujibu mara moja.

Lakini baada ya sekunde chache, alisema:

“Watu wa ndani…”

Kedmund alishtuka.

“Ndani? Unamaanisha… Rashid?”

Amina alinyamaza.

Hiyo ilikuwa jibu tayari.

Walijificha nyuma ya jengo moja lililotelekezwa.

Pumzi zao zilikuwa nzito.

Kedmund alimtazama Amina kwa mshangao.

“Unajua kila kitu… sivyo?”

Amina alifumba macho kwa sekunde.

Kisha akasema kwa sauti ya chini:

“Kedmund… kuna kitu sijakuambia.”

Moyo wake ulianza kuzama.

“Kitu gani?”

Amina alimwangalia…

Na hapo ndipo ukweli ulianza kutoka.

“Mimi… sikuwekwa karibu na wewe kwa bahati mbaya.”

Kimya kilitanda.

“Kuna watu walinituma… nikukaribie… nikujue… na nikulete karibu.”

Kedmund alihisi dunia ikisimama.

“Unamaanisha… haya yote…?” sauti yake ilitetemeka.

Amina hakujibu moja kwa moja.

Lakini macho yake yalikuwa yamejaa majuto.

Sekunde chache za ukimya zilikuwa nzito kuliko kelele yoyote.

Kedmund alicheka kidogo… lakini haikuwa furaha.

“Ilikuwa mchezo… sio?”

Amina alisogea karibu.

“Ilianza hivyo… lakini sasa—”

“USISEME!” Kedmund alipaza sauti.

Macho yake yalikuwa yamejaa hasira na maumivu.

“Usijaribu kuniambia ni kweli sasa!”

Moyo wake ulikuwa umevunjika.

Sio kwa sababu ya hatari…

Bali kwa sababu ya usaliti.

Lakini kabla mambo hayajaenda mbali—

🔫 SAUTI YA RISASI!

Ukuta karibu nao ulipasuka.

“Wamewafikia!” Amina alipaza sauti.

Hakukuwa na muda wa drama tena.

Walilazimika kukimbia tena.

Lakini safari hii…

Kedmund hakuwa anakimbia tu kwa ajili ya maisha yake.

Alikuwa anakimbia kutoka kwa mtu aliyemuumiza.

Ndani ya moyo wake, kitu kilikuwa kimevunjika kabisa.

Na kitu kipya kilikuwa kinazaliwa…

👉 Hasira.

👉 Kutoamini mtu yeyote.

👉 Na tamaa ya kujua ukweli wote… hata kama utamuumiza zaidi.


Mwisho wa Sehemu ya 5


#Like_comment Tuendelee sehemu 6.

Comments

Popular posts from this blog

SEHEMU YA KWANZA

SEHEMU YA SITA