SEHEMU YA PILI
SEHEMU YA 2 Asubuhi ilipochomoza, jua lilitoa mwanga hafifu juu ya kijiji cha Mlimani. Kila kitu kilionekana cha kawaida… lakini si kwa Zuberi. Usiku ule haukutoka kichwani mwake. Aisha. Sauti yake… macho yake… na maneno yake ya kutisha: “Yeyote anayenipenda… hufa.” Zuberi aliketi nje ya nyumba yao, akitazama ardhi kwa mawazo mazito. Hakula, hakulala vizuri. Moyo wake ulikuwa umefungwa na kitu kisichoeleweka. “Zuberi, kuna nini?” sauti ya rafiki yake Jamal ilimkatisha mawazo. Zuberi alimwangalia, akasita kidogo, kisha akasema, “Jamal… ukiambiwa kuna mtu hawezi kugusa ardhi… utaamini?” Jamal alicheka kidogo. “Wewe umeanza tena hadithi zako za usiku?” “Hapana… naongea ukweli.” Zuberi alimuelezea kila kitu—mwanga, msitu, na msichana aitwaye Aisha. Lakini kadri alivyoongea… uso wa Jamal ulibadilika. Hakuwa tena anacheka. “Umemuona… kweli?” aliuliza kwa sauti ya chini. Zuberi alishangaa. “Unamjua?” Jamal alinyamaza kwa sekunde kadhaa… kisha akasema kwa sauti ya hofu: “Kama huyo ni Aish...